Kabla hatujaangalia ni jinsi gani mtu anaweza kupata mafanikio katika maisha yake kama ni vyema tukaangalia nini maana ya mafanikio:-
MAFANIKIO NI NINI?
Je unazani mtu aliyefanikiwa nin Yule mwenye majumba,magari na elimu ya kutosha laa! Hapana bali mafanikio tunaweza kuangalia maana yake kwa vupengele vifuatavyo:
(1)Kuwa na mtazamo chanya.
(2)kuwa na uhusianao mzuri na watu.
(3)kuishinda hofu.
(4)kupenda kwa vitendo.
(5)kubariki wengine unapobarikiwa.
(6)kuwa na imani inayoonekana.
(7)Kuwa na usalama wa kipato.
Ø KUWA NA MTAZAMO CHANYA
Maana moja wapo ya mafanikio ni ile hali ya mtu kuwa na mtazamo chanya katika maisha yake kwa mfano mtu anapojiamini kuwa anaweza kufanya jambo alilolikusudia kulifanya kwa wakati Fulani tunasema amefanikiwa kwasababu amekuwa na mtazamo chanya kwani alijiamini anaweza kwa hilo hiyo nayo ni njia mojawapo ya mafanikio
Ø KUWA NA UHUSIANO MZURI NA WATU
Vilevile mafanikio ni ile hali ya mtu kuwa na mahusiano mazuri na watu waliomzunguka katika jamii yake kwa mfano mtu ambae anamahusiano mazuri na watu pale anapopatwa na tatizo inakuwa ni rahisi kusaidika tofauti na mtu ambae mahusiano yake na watu wengine hayajakaa vizuri au ni mabaya kwa iyo tunaona kuwa mahusiano mazuri baina ya watu katika jamii ni mafanikio
Ø KUISHINDA HOFU
Kwa kawaida kila binadamu ana hofu zake kuna hofu za aina mbalimbali watu wengine wano hofu ya kifo,hofu ya umaskini,hofu ya magonjwa,hofu ya ajali n.k ili tuweze kutambua kuwa mtu amefanikiwa ni lazima mtu huyo azishinde hofu za maisha na kusonga mbele kwa iyo maana nyingine ya mafanikio ni kuishinda hofu tunazokabiliana nazo katika maisha yetu ya kila siku na ni muhimu kujua kuwa mungu yupo pamoja hata katika magumu
Ø KUPENDA KWA VITENDO
Mtu aliyefanikiwa upendo wake upo kwenye vitendo yaani anakuwa na upendo unaoonekana,uwezi kusema umefanikiwa katika maisha yako kama utakuwa unachuki ndani yako zidi ya mtu mwingine,hivyo ni v yema kama tunataka kufanikiwa tuonyeshe upendo wetu kwa watu wengine kwa vitendo,kwa hiyo mafanikio pia ni ile hali ya mtu kuwajali na kuwa penda watu wengine wanaomzunguka katika jamii yake
Ø KUBARIKI WENGINE UKIBARIKIWA
Maana nyingine ya mafanikio ni hali ya kuwakumbuka wale wahitaji na kuwasaidia pale unapobarikiwa. Sikuzote mtu aliyefanikiwa kikwelikweli si mchoyo wa kuwapa Baraka wale ambao wapo kwenye uhitaji,kwa mfano unamwona mtu amefanikiwa yaani anafedha za kutosha lakini awakumbuki wenye uhitaji basi huyo mtu ajafanikiwa kwa sababu hajui kuwa mungu ndie anaewapa watu nguvu za kupata utajiri
Ø KUTOKATA TAMAA {DON’T GIVE UP}
Mafanikio pia ni hile ali ya mtu ya kusonga mbele pasipo kukata tamaa katika maisha yake. Ili uweze kufanikiwa katika maisha yako ni lazima uwe jasiri unatakiwa usiogope kujaribu kufanya chochote kitakachoweza kukuvusha kutok hatua moja kwenda nyingine,na zifanyie kazi fursa zozote za kimaendeleo zinazokuja mbele yako.
Ø KUWA NA USALAMA WA KIPATO
Vilevile mafanikio pia tunaweza kusema ni hile hali ya mtu kuwa na usalama wa kipato yaani anayo akiba kidogo kwa ajili ya dharura inapotokea.
-siku zote watu ambao wamefanikiwa huwa na akiba hawatumii fedha zao kabla ya mpango alioudhamiria na pia hawatumii zaidi ya kile wanachokipata kwa mfano unaweza ukamkuta mtu anapewa mshahara wa laki tano [500,000] na anatumia laki sita [600,000] hii inamaanisha huyu mtu anausalama wa kipato kwasababu anatumia zaidi ya kile anachokipata kwa hiyo kuendelea kwako itakuwa ni vugumu.
NJIA YA KUPATA MAFANIKIO KAMA KIJANA
Zifuatazo ni njia ambazo zinaweza kukusaidia kupata mafanikio kama kijana
v JITAMBUE WEWE NI NANI NA UTATAKA NINI KTK MAISHA YAKO
-Njia mojawapo ya kufanikiwa ktk maisha yako ni lazima ujitambue wewe ni nani na unataka nini ktkl maisha yako, vijana wengi wanapotea na kuanza kulalamika kwasababu hawajajitambua, ukishajitambua ni kwanini mimi ninaishi mpaka sasa hivi wakati kunavijana wa rika langu ambao wamekufa na wengine ni wagonjwa,utajua linalokupasa kufanya ktk maisha yako.
v KUJUA NYAKATI AU WAKATI SAHIHI
-Pia ili mtu aweze kufanikiwa lazima ajue anaishi ktk nyakati zipi na ni mambo gani ambayo yanampasa kuyafanya, ili tuweze kufikia malengo yetu kama vijana na lazima tufanye mambo kwa wakati sahihi, kwa mfano kama ni wakati wa kusoma, soma na kama ni wakati wa kufanya kazi fanya tena kwa bidii.
v KUTUNZA NA KUTUMIA WAKATI VIZURI
-Ili tuwe kufanikiwa ktk maisha yetu kama vjana ni vyema kutunza na kutumia mda wetu vizuri,ili uweze kufanikiwa lazima utumie wakati vizuri kwasababu mda ni zawadi au Baraka iliyotoka kwa mungu
-Kumbuka unachokipata leo ndio tafsiri ya kesho yako itakuwaje, kwa hiyo tuwe makini ktk utumiaji wa mda. Kuna baadhi ya watu ambao hawautumii mda wao vizuri,
-Mambo yanayoweza kusababisha mtu asiutumie mda wake vzuri
ü Kutokuwa na malengo katika maisha yako
-Hii inasababisha mtu asitumi mda wake vizuri kwasababu hanavipaumbele ktk maisha yake.yaani anaishi ili mradi maisha yaende na siku zisogee.
ü Kairisha mambo
-Unaweza ukamkuta mtu amepanga mambo yake lakini anayahairisha hivyo anajikuta anautumia mda wake vibaya.
ü Kukosa utulivu na maamuzi ya kufanya kitu kimoja baada ya kingine
-Hii nayo inasababisha mtu asitumie mda wake vizuri ktk maisha yake ya kila siku.
v KUWA NA MALENGO
Njia mojawapo ya kufanikiwa ni kujiwekea malengo ktk maisha yako kwasababu pasipo malengo maisha ya mtu hayana muelekeo, hivyo ni vyema kujiwekea malengo na kuhakikkisha unayafikia na usipo yafikia ujiwekee mikakati ya kuweza kuyafikia mda unaofuata .
v KUWA NA TABIA YA KUJIDHAMINI
Njia mojawapo ya kufanikiwa ni kupenda kijidhamini,ni vyema kila siku utafakari kwa mfano tangu siku ilipoanza nimefanya mangapi yenye tija na ambayo yatanivusha kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine kiuchumi, kimawazo n.k
-Kwa hiyo kujidhamini kwako kutakuonyesha kama unarudi nyuma kimaendeleo, au uko palepale au unasonga mbele.
v KUCHAGUA MARAFIKI WAZURI
Njia mojawapo ya kuweza kufanikiwa ni kuwa na marafiki ambao watakuwa sambamba na wewe kufikia malengo yako kwasababu marafiki wanauwezo mkubwa kudetermine future yako, kwa hiyo kuwa makini sana pale unapochagua marafiki ili uweze ku
kufanikiwa.jinsiyakupatamafanikiokijana